Ushawahi kuona mtu anajenga jela yake mwenyewe na kuiremba kisha
kuchagua magereza wa kumlinda, mtu alieogopwa na wauza madawa wenzake na
kuwaweka majaji, polisi na wanasiasa mfukoni kwa pesa ama vitisho. Moja
ya watu wakatili aliemuondoa yoyote aliekuwa kikwazo katika njia yake
akiwa na sera ya aidha ukubali rushwa au risasi za Pablo.
Anaitwa Pablo Escobar a.k.a El Doctor, El Patrón,Don Pablo,El Señor, El
Magico.
Kila $1 aliyokua anaweka katika biashara yake alikua anapata profit OR
return ya $200.
Alikuwa anakusanya pesa haweki bank, anatunza ndani chini ya ardhi, juu
ya dari or ukutani. Adui pekee wa hela zake walikuwa ni Panya wenye njaa
kali. Kila mwaka inasemekana alikua anapoteza 10% ya faida ambayo kwa
haraka haraka ni $b1, Panya
walizokuwa wanakula.
Marekani na Serikali ya Colombia ilitaka Pablo akamatwe na afungwe.
Akakubali but Gereza akajenga yeye. Ndani ya gereza kulikuwa ni kama
5star hôtel. Alijiwekea kila kitu, Jacuzi, Bar, Pub, TV,na vitu kibao
vya thamani. Pia wanawake wakawa wanaingia na akiwa jela alikuwa ana
uwezo wa kutoka na kurudi kisirisiri, coz walinzi wa gereza alikuwa
anawahonga vizuri sana.
Baadae, Pablo alichoka maisha ya Jela la Hôtel, anataka kurudi kitaa,
akatoroka. Wakati anatoroka akachukua familia yake na walinzi wake
wakakimbilia Maporini. Wakati wapo huko vichakani, mtoto akaugua ghafla
na kukawa na baridi sana, ukahitajika moto unajua Pablo alochofanya?
Aliwasha moto wa kutoa baridi la ugonjwa wa kwa mwanae kwa kutumia noti
zaidi ya 2million dollars, ziliwasha moto mtoto aote moto kupata joto,
na kupika kwa note za $2,000,000, za kibongo ni b3 na m240.
Alikuwa ananunua na kutumia Rubber band za $2,500 = tsh 4,050,000 za
kibongo kufungia hela zake kila mwezi, so kwa mwaka alikuwa ananunua
rubber band za $30,000 = 48,600,000 kufunga tu mihela yake (hata BOT
hawatumii rubber band za $2,500 kwa mwezi na haijawahi kutokea kwa mtu
wala taasisi)
Alinunua ndege kwa ajili ya kusafirishia hela zake tu, kila trip ndege
ilikuwa inabeba $10m. Mwaka 1989, Forbes ilimtaja kama tajiri wa 7
duniani, anakadiriwa kuwa na utajiri wa $25-30b, watu wake wa karibu
wanasema alikuwa anazidi hata hapo coz kwa siku alikuwa anatengeneza sio
chini ya $60m, coz kwa mwezi alikuwa anasafirisha zaidi ya 80-100t USA.
Na ubabe wake wote, Pablo alikuwa anaogopa sana kufa. Baada ya kutoroka
Jela, serikali na jeshi la Colombia wakawa wanamtafuta Pablo,
akawa-offer serikali iachane nae na atailipia serikali deni ililokuwa
inadaiwa $b10 zaidi ya tirioni 18 za kibongo, ili serikali imalize deni
inalodaiwa, lakini serikali ilikataa, msako wa Pablo wakakabidhiwa
wamarekani na kumuua December 2/1993.
Mpaka leo hongo/rushwa kubwa duniani kuwahi kutokea ni hiyo ya $10b ya
Pablo kutaka kulipa deni la taifa la Colombia, 10b usd = trilioni 18.
Saturday, May 14, 2016
Home »
tukio
» MFAHAMU PABLO ESCOBAR,GOD FATHER WA MADAWA YA KULEVYA ALOACHA HISTORIA YA PEKE YAKE DUNIANI




0 comments:
Post a Comment