Friday, May 27, 2016

M 2The P aeleza kilichotokea siku Ngwea anafariki, adai anahisi kuna mkono wa mtu

Msanii wa muziki M 2The P ambaye alikuwa rafiki mkubwa wa msanii Albert Mangwea, amesema hadi leo anahisi kuna mtu aliyehusika na kifo cha Ngwea, na kumfanya ashindwe kuamini ni ajali ya kawaida.

MSANII M 2THE P AKIWA NA HAYATI NGWAIR

Akiongea katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio Ijumaa hii, M2The P amesema kitendo cha kuibiwa vitu vyao vyote ndio kilichompa wasi wasi.
“Unajua ile siku tuli-party sana,” alisema M2 The P. “ Tumepiga bata lakini kilichonishtua, ni sawa tukio lilikuwa kama ilivyoonekana ila kilichonishangaza ni baada ya kurudi ghetto tukakuta vitu vyote vimeibiwa, kitu kilichonishtua, ina maana ilikuwa ni kama walitu-target kabisa,”
Pia msanii huyo ambaye naye siku ya tuko hakuwa katika hali nzuri baada ya kupoteza fahamu, amesema kulingana na hali hiyo, anaunga mkono kauli ya mama mzazi wa Ngwea Bi. Denisia Constantino, kwamba huenda kuna watu walishiriki kusababisha kifo cha Ngwea.

Friday, May 20, 2016

Diamond kwenye headlines nyingine na Wizkid, AKA, Drake, Beyonce na Rihanna

   
   
May 20 2016 Tanzania imeamka na habari nyingine njema za Diamond Platnumz kuchaguliwa tena kushiriki kwenye tuzo za kituo maarufu cha TV Marekani kiitwacho BET ambapo Platnumz amekua na mwaka mwingine mfululizo wa kuwa nominated na sasa ni kwenye tuzo za BET Awards 2016.
Diamond ameshukuru kwa kuchaguliwa kuwania tuzo kwenye kipengele cha Best international Act Africa ambapo ameyaandika maneno haya baada ya kufikiwa na taarifa >>> ‘Ningependa niwashukuru kwa Sapoti kubwa Manayozidi kunipa na niwajuze kuwa kijana wenu nimechaguli kuwania tunzo ya Msanii Bora wa Kimataifa toka Africa kwenye tunzo za BET #BETAwards America’
Tuzo za BET 2016 ambazo zitatolewa nchini Marekani zimeanza kuchukua nafasi kwenye headlines baada ya kutangazwa list ya waliochaguliwa kuwania huku Beyonce, Rihanna na Drake wakitangazwa kuongoza kwa kuwania tuzo zaidi ya moja.






  BET 2

Wednesday, May 18, 2016

MANENO YA PELE: Pele asema kama yeye ni mfalme basi Messi ni Prince.

   

Trump: Ninaweza kuzungumza na Kim Jong-un

    
    
Mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amesema yuko tayari kufanya mazungumzo na kiongozi wa Korea Kaskazini kuhusu mpango wa nyuklia wa taifa hilo.
“Ninaweza nikazungumza naye, Siwezi kuwa na tatizo kuzungumza naye,” Bw Trump alisema kuhusu Kim Jong-un.
Mkutano huo ungekuwa tofauti kabisa na msimamo wa muda mrefu wa Marekani kuhusu Korea Kaskazini.
Hatua hiyo imemfanya mgombea anayeongoza katika kinyang’anyiro cha chama cha Democratic Hillary Clinton kumshutumu Bw Trump na kusema anashangaza kwa kuwaenzi sana viongozi wababe wan chi za nje.
Taarifa iliyotolewa na mmoja wa wasaidizi wa Bi Clinton imesema sera ya mambo ya nje ya Bw Trump usio wa maana yoyote.

>>>>Kwingineko, BBC imefahamu kwamba huenda Bw Trump akazuru Uingereza kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini Marekani mwezi Novemba.
Wanadiplomasia wanatarajia ziara hiyo ifanyike baada yake kuwa rasmi mgombea urais wa chama cha Republican mwezi Julai.
Mapema wiki hii, Bw Trump alisema dalili zinaonesha huenda asiwe na uhusiano mwema sana na Uingereza.
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron na meya mpya wa London Sadiq Khan, ambaye ni Mwislamu, wamemshutumu Bw Trump kutokana na hatua yake ya kupendekeza Waislamu wazuiwe kuingia Marekani.


Tuesday, May 17, 2016

Mambo usiyoyajua kuhusu Korea Kaskazini.....

.
1.Bangi ni Halali kabisa nchi nzima, na haichukuliwi kama ni kitu cha kulewesha /drug.
2.Ndio nchi pekee duniani hadi sasa amabayo imewahi kuiteka meli ya kivita ya wamarekani.
3.Wakati dunia nzima leo ni 2016 kwao ni mwaka 105 wakihesabu kuanzia kifo cha kiongozi wao Kim il-Sung
4.Kuanzia 2009 nchi hii sio ya kikomunist tena, wana msimamo au IDEOLOGY yaoo mpya unaitwa " JUCHE"
5.Ndio nchi yenye uwanja mkubwa wa mpira kuliko yote dunia nzima, unabeba watu 150000
6.Miaka ya 50, walijenga mji fake (nice city) mpakani ili kuwavutia watu wahamie kutoka south korea.
7.Kunyoa Nywele, unaoption ya kuchagua kati ya style 28 zilizopitishwa kitaifa nje ya hapo ni kosa kisheria.
8:Kwa miaka 60 iliyopita ni wakorea kaskazini 23,000 waliokimbilia Korea Kusini wakati ni wakorea kusini wawili tu ndio wamerudi korea kaskazini.
9:Wakati dunia nzima inatumia OS za Windows,LINUX au MAC OS etc , wao wanatumia ya kwao inaitwa STAR OS
10:Kumiliki BIBILIA,Kuangalia Movie au tamthilia za Korea kusini na kusambaza picha za ngono adhabu ni kifo ukibainika.
11:Ni wanajeshi na viongozi wa serikali tu ambao wanaruhusiwa kumiliki gari.
12:Ni kinyume cha sheria kuvaa jeans korea kaskazini
13:Wanafanya uchaguzi kila baada ya miaka mitano ila sanduku la kura ni moja tu na mgombea ni mmoja.
14:Kuna Shirika Linalotumia parachuti kuzipeleka BIBILIA nchini humo wakiomba angalau ziangukie kwa mmoja aelewe neno.
15:Kulingana na vitabu vya nchi hiyo Kiongozi wao Kim Jong Un alijifunza kuendesha gari akiwa na miaka 3.
16: kama umezaliwa tarehe 8 july au tarehe 17 december Huruhusiwi kusherekea Birthday maana ni siku ambazo viongozi wao Kim Jong Il na Kim Il song walikufa.
17: wanamiliki kikosi maalumu cha wanajeshi wanaakili sana/geneus kama jeshi la kimtandao,Special cyber hackers, Unit 121 au Beaureu 121. Na inasemekana wametuma baadhi yao zaidi ya askari hao 1200 nchi mbalimbali kwa mashambulizi au cyber war. Ndio waliohusika katika Shambulizi la Kampuni ya SONY Klingana na vyombo vya magharibi.

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imeomba kutengewa Trilioni 4 kama bajeti yake ijayo


Bunge la 11 limeendelea Dodoma, na leo May 17 2016 ilikuwa ni zamu ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuwasilisha hotuba yake pamoja na kuomba kupitishiwa bajeti yake ijayo.  Kazi imefanywa na Waziri  wake Makame Mbarawa ambaye ameanza na kuzitoa changamoto za Wizara…

>>‘Katika utekelezaji wa majukumu yake Wizara inakabiliwa na changamoto mbalimbali, changamoto hizo ni pamoja na upungufu wa fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo, uzidishaji wa uzito wa magari ya mizigo unaosababisha uharibifu wa barabara

Msongamano wa magari katika jiji la Dar es salaam, uvamizi wa maeneo ya Hifadhi ya Barabara na Reli, kujenga uwezo wa Makandarasi wazalendo katika kutekeleza miradi ya maendeleo, ajali za barabarani, wizi wa miundombinu ya uchukuzi kutokana na biashara ya chuma chakavu n.k
Mwisho Waziri Mbarawa akaomba fedha…>>>Katika mwaka 2016/2017, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inaomba kuidhinishiwa jumla ya Shilingi 4,895,279,317,500.00’. Kati ya fedha hizo, Shilingi 2,212,141,496,500.00 ni kwaajili ya Sekta ya ujenzi

Shilingi 2,587,333,762,000.00 ni kwa ajili ya Sekta ya Uchukuzi na Shilingi 95,804,059,000.00 ni kwa ajili ya Sekta ya Mawasiliano ‘

UNGANA NAMI KISHEY PLTNUMZ SASA!

TWITTER, FACEBOOK, INSTAGRAM

Saturday, May 14, 2016

Ice Boy kutoka ‘High Table Sound’ ya Barnaba azungumzia mipango ya muziki wake

Msanii wa muziki kutoka label ya ‘High Table Sound’ ya Barnaba, ‘Ice Boy’ amefunguka na kuzungumzia maisha yake ya muziki pamoja na mipango yake akiwa ndani ya label hiyo.


Akizungumza na Bongo5, Ice Boy amesema anaamini ‘High Table Sound’ inaweza kubadili maisha yake ya muziki.“Kwa sasa nipo kwa Barnaba, tayari nimeona wapi natakiwa kwenda na kwa njia gani,” alisema Ice Boy. Kwa hiyo naweza sema hapa kwangu ni sehemu sahihi kwangu, tayari kuna kolabo za kimataifa nimefanya, kwa hiyo mashabiki wakae mkao wa kula kuna mambo mengi mazuri yanakuja,” alisema Ice Boy.

NDANI YA MIEZI MICHACHE MSANII 2FACE IDIBIA AMESAINI DILI HILI JINGINE JIPYA..

BAHATI YA MWENZIO USIILALIE MLANGO WAZI:

 
2Face Idibia asaini dili la tatu kama balozi ndani ya miezi michache.
Hatua hiyo imekuja baada ya wiki iliyopita kupata shahada ya heshima kutoka chuo kikuu cha Igbinedioncha nchini Nigeria na kuwa msanii wa kwanza wa nchi hiyo kupatiwa tuzo ya heshima kama hiyo.
Mwaka 2016 umeonekana kuwa wa neema zaidi kwa hitmaker huyo wa ‘African Queen’ baada ya kusaini mkataba mwingine na kampuni ya simu, Partner Mobile.

Baadhi ya wasanii wa nigeria waliosaini mikataba tofauti tofauti ni Davido akisaini na Pepsi Niger, Flavour na Banky W.

MFAHAMU PABLO ESCOBAR,GOD FATHER WA MADAWA YA KULEVYA ALOACHA HISTORIA YA PEKE YAKE DUNIANI

     Ushawahi kuona mtu anajenga jela yake mwenyewe na kuiremba kisha kuchagua magereza wa kumlinda, mtu alieogopwa na wauza madawa wenzake na kuwaweka majaji, polisi na wanasiasa mfukoni kwa pesa ama vitisho. Moja ya watu wakatili aliemuondoa yoyote aliekuwa kikwazo katika njia yake akiwa na sera ya aidha ukubali rushwa au risasi za Pablo. Anaitwa Pablo Escobar a.k.a El Doctor, El Patrón,Don Pablo,El Señor, El Magico. Kila $1 aliyokua anaweka katika biashara yake alikua anapata profit OR return ya $200. Alikuwa anakusanya pesa haweki bank, anatunza ndani chini ya ardhi, juu ya dari or ukutani. Adui pekee wa hela zake walikuwa ni Panya wenye njaa kali. Kila mwaka inasemekana alikua anapoteza 10% ya faida ambayo kwa haraka haraka ni $b1, Panya

walizokuwa wanakula. Marekani na Serikali ya Colombia ilitaka Pablo akamatwe na afungwe. Akakubali but Gereza akajenga yeye. Ndani ya gereza kulikuwa ni kama 5star hôtel. Alijiwekea kila kitu, Jacuzi, Bar, Pub, TV,na vitu kibao vya thamani. Pia wanawake wakawa wanaingia na akiwa jela alikuwa ana uwezo wa kutoka na kurudi kisirisiri, coz walinzi wa gereza alikuwa anawahonga vizuri sana. Baadae, Pablo alichoka maisha ya Jela la Hôtel, anataka kurudi kitaa, akatoroka. Wakati anatoroka akachukua familia yake na walinzi wake wakakimbilia Maporini. Wakati wapo huko vichakani, mtoto akaugua ghafla na kukawa na baridi sana, ukahitajika moto unajua Pablo alochofanya? Aliwasha moto wa kutoa baridi la ugonjwa wa kwa mwanae kwa kutumia noti zaidi ya 2million dollars, ziliwasha moto mtoto aote moto kupata joto, na kupika kwa note za $2,000,000, za kibongo ni b3 na m240. Alikuwa ananunua na kutumia Rubber band za $2,500 = tsh 4,050,000 za kibongo kufungia hela zake kila mwezi, so kwa mwaka alikuwa ananunua rubber band za $30,000 = 48,600,000 kufunga tu mihela yake (hata BOT hawatumii rubber band za $2,500 kwa mwezi na haijawahi kutokea kwa mtu wala taasisi) Alinunua ndege kwa ajili ya kusafirishia hela zake tu, kila trip ndege ilikuwa inabeba $10m. Mwaka 1989, Forbes ilimtaja kama tajiri wa 7 duniani, anakadiriwa kuwa na utajiri wa $25-30b, watu wake wa karibu wanasema alikuwa anazidi hata hapo coz kwa siku alikuwa anatengeneza sio chini ya $60m, coz kwa mwezi alikuwa anasafirisha zaidi ya 80-100t USA. Na ubabe wake wote, Pablo alikuwa anaogopa sana kufa. Baada ya kutoroka Jela, serikali na jeshi la Colombia wakawa wanamtafuta Pablo, akawa-offer serikali iachane nae na atailipia serikali deni ililokuwa inadaiwa $b10 zaidi ya tirioni 18 za kibongo, ili serikali imalize deni inalodaiwa, lakini serikali ilikataa, msako wa Pablo wakakabidhiwa wamarekani na kumuua December 2/1993. Mpaka leo hongo/rushwa kubwa duniani kuwahi kutokea ni hiyo ya $10b ya Pablo kutaka kulipa deni la taifa la Colombia, 10b usd = trilioni 18.


Eti kuna sehemu Kanye West akiwepo,huruhusiwi kumtazama,ni lazima utazame pembeni.

 
Muhudumu wa chakula maarufu Mjini New Yori Stacy Adler ’50’ amefunguka juu ya kitendo alichofanyiwa wakati wa shughuli ya Kanye West na kusema nikitendo ambacho hata sahau.
Kwenye kitabu kipya cha Ina Yalof ‘Food and the City’ muhudu huyu anayefanya kazi na mastaa wengi kama Beyonce, Jay Z, Jennifer Lopez, George Clooney, Madonna amesema aliambiwa asimtazame Kanye West na kwamba wakati anapita wahudumu wote waangalie pembeni.
Stacy anasema”Watu wote maarufu wako powa sana ila wapambe wao ndio wanasumbua, niliambiwa na watu wa Kanye kuwa akipita hakuna mtu wa kumtazama, lazima uweke shingo pembeni na usimuone wakati anapita kitu ambacho kilinikera sana“.

Sports Louis van Gaal anategemea kuwepo na Man United msimu ujao.



 

Louis van Gaal anasema yeye anafikiria atakuwepo na klabu ya Manchester United mpaka msimu ujao na atabaki kuwa meneja wa klabu hio.
Louis Van Gaal anategemea kumalizia miaka mitatu ya mkataba wake aliosaini na klabu hio mwaka 2014.
Louis anasema  “I have said I shall be here, that is my opinion, so the board has to decide if it is like that.”
Van Gaal amekuwa na presha toka mwezi December mwaka jana huku aliyekuwa kocha wa Chelsea manager Jose Mourinho ametajwa kuwa na maongezi ya kuchukua mikoba yake hapo Man United.

 Ungana nami Kishey Platnumz sasa
Jiunge nami kupitia Facebook, twitter na Instagram upate update za kijanja!

NJOO UCHEKE NA UMTAG MWENZIO KWENYE COMMENT

Inakuaje mtu wangu, ebu niambie enzi zako ulikuwaje kwenye hii video wala usione aibu video nimekuwekea chini hapa !!









BADAE  KIDOGO









Mtoto wa Michael Jackson aanza kufuata nyayo za baba yake

Mtoto wa nyoka ni nyoka tu.

                                                                        PRIS JACKSON
 
Hatimaye mtoto wa Michael Jackson, Pris Jackson (18) ameanza kufuata nyayo za baba yake kwa kuanza kutoboa ulimi. Paris amepost picha inayomuonyesha akiwa ametoboa ulimi na kuweka kipini na kuandika: “almost like ring-toss. but with noodles and needles.”
Miaka kadhaa nyuma kabla ya kufariki, Michael Jackson aliwahi kujibadili muonekano wake wa ngozi na kuzua maswali mengi kwa mashabiki duniani.

 Ungana nami Kishey Platnumz sasa
Jiunge nami kupitia Facebook, twitter na Instagram upate update za kijanja!

Friday, May 13, 2016

Hatuangalii ukubwa wa jina la msanii - Mafikizolo

kundi la muziki kutoka South Afrika Mafikizolo wamesema kolabo inaweza kumyanyua mtu katika muziki na kufanya akawa na nafasi nzuri kimataifa kwa hiyo kolabo ni kitu kizuri kwa wasanii.

                                          kundi la muziki kutoka South Afrika Mafikizolo
 
     
Wakizungumza na Enewz Mafikizolo wamesema kuwa kwa wasanii wanaohitaji kolabo na kundi lao wao hawaangalii ukubwa wa jina la msanii bali wanachokiangalia radha ya msanii na uwezo wa mtu katika kuimba.
“Huwa hatuangalii jina la msanii sisi tukipenda tu radha ya msanii tunafanya nae kolabo na hivyo ndivyo wasanii wengine wanapaswa kuviangalia”,walisema Mafikizolo.
Huku wakitolea mfano walivyowapa nafasi uhuru na Maphorisa na kuwaweka juu katika ramani ya muziki wakati walikuwa hawatambuliki katika game ya muziki lakini wao waliweza kuwafanya wao kutambulika na wengine kuanza kuomba kolabo kwao.

Ungana nami Kishey Platnumz sasa
Jiunge nami kupitia Facebook, twitter na Instagram upate update za kijanja!

Mwanamke mkongwe zaidi duniani afariki New York

Mwanamke aliyetambuliwa kuwa mkongwe zaidi duniani ameaga dunia akitibiwa jijini New York, Marekani, madaktari wamesema.
Susannah Mushatt Jones, amefariki akiwa na umri wa miaka 116.

      Alizaliwa eneo la mashambani jimbo la Alabama mwaka 1899, na amekuwa akiugua kwa siku kadha.

Ungana nami Kishey Platnumz sasa
Jiunge kupitia twitter, facebook na instagram upate update za kijanja!

Mwanamuziki apigwa marufuku na Twitter


Mwanamuziki wa mtindo wa Rap Azealia Banks amepigwa marufuku na mtandao wa Twitter.
Nyota huyo wa 212 amezuiliwa kuingia katika mtandao huo kufuatia hatua yake ya kutumia mtandao huo kumtusi msanii Zayn Malik.
Ameshtumiwa kwa ubaguzi baada ya kufananisha mizizi ya mwanamuziki huyo mbali na kutumia matusi.


Kufuatia matamshi yake dhidi ya Zayn,ameondolewa katika tamasha la Born and Bred mjini London.
Gazeti la Metro limeripoti kwamba wizara ya maswala ya ndani nchini humo ilikuwa na mpango wa kumpiga marufuku mwanamuziki huyo kutoingia Uingereza.
Ukurasa wake wa Twitter kwa sasa unaonyesha kwamba amepigwa marufuku na kwamba akaunti yake imeondolewa katika mtandao huo.

Ungana nami Kishey Platnumz sasa
kupitia facebook, twitter na instagram upate update za kjanja!

Youtube sasa kuanza kutumika kama app ya kutumiana ujumbe

YouTube inatengeneza mfumo wa kutuma ujumbe na kusambaza vitu kwenye mifumo ya simu ya Android na iOS katika jaribio la kuwabakiza watumiaji wake wanaotazama video hapo hapo.


Tofauti na vitu vilivyopo sasa vya kuweka ujumbe na kusambaza, mfumo huo utakuwa zaidi wa kusambaza video ndani kwa ndani na kuchat na marafiki au kundi fulani. Tab mpya ya kushare itaonekana kwenye app ya simu itakayokuwa na video ulizoshare na mazungumzo na watu wako.
Utaweza kuandika ujumbe na kuweka emoji kama app zingine za kuchat na unaweza kulike comments, kuongeza marafiki kwenye kundi na kuangalia video zilizosambazwa na marafiki zako.
 Huduma hiyo kwa sasa ipo kwa watu wachache tu.


Ungana nami Kishey Platnumz sasa.
 Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town!

Picha,Drake na French Montana wanaitayarisha collabo yao.

Kushoto ni rapa Drake, katikati Rapa Frenchi Montana wakiwa na Producer
 Noah "40" Shebib

 
Drake na French Montana wanaelekea kukamilisha collabo yao mpya baada ya kukalisha kinoma kwenye colabo zao kama “Pop That” na “Stay Schemin.” Montana na Drake walikuwa studio hivi karibuni kufanya kazi pamoja.

                  Drake na French Montana wakiwa na washkaji studio
Ungana nami Kishey Patnumz sasa.
 Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town!

Thursday, May 12, 2016

CLAUDIO RANIERI ACHAGULIWA KUWA KOCHA BORA MWAKA 2016

Kocha wa klabu ya Liecester City Claudio Ranieri achaguliwa kuwa kocha bora mwaka 2016 na kunyakuwa tuzo ya Enzo Bearzot inayotolewa na shirika la soccer nchini Italia.


Ranieri amejipatia tunzo hiyo baada ya kuisadia timu yake ya Leicester City kutoa ubingwa wa ligi ku ya Uingereza kwa mara ya kwanza katika historia ya timu hiyo
Tuzo hizo zilianza kutolewa mwaka 2011 na shirika la soka Italia.


Jiunge na Kisheyplatnumz  sasa

Usipitwe!! Jiunge nami kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! 

PICHA ZA GARI MPYA YA NUH MZIWANDA ALIYOPEWA NA USIMAMIZI WAKE MPYA.


Bongo fleva super staa Nuh Mziwanda amezawadiwa gari mpya na usimamizi wake mpya unaojiita LFLG maana yake ikiwa ni Living Fast Living Good.
Usimamizi huu yupo Petit Money, Hydary pamoja na GEE Model anayeshughulikia swala la mavazi.

Picture 1

Picture 2

Picture 3

Picture 4

Picture 5

PICHA 7:Kilivyohappen kwenye birthday party ya meneja wa Diamond Platnumz…mafikizolo wahudhuria


May 11, 2016 meneja wa mwimbaji staa wa bongofleva Diamond Platnumz, Sallam alisherehekea siku yake ya kuzaliwaDar es salaam na wadau mbalimbali wa muziki wa Bongo Fleva huku ikiwa imehudhuriwa na  wasanii kutoka Afrika Kusini Mafikizolo.></
div>

BREAKING NEWS: INSTAGRAM KUANZA KUTUMIA NEMBO MPYA

Instagram imezindua nembo mpya katika hatua ya kutaka kujiboresha na kutoonekana kuwa programu ya picha pekee.




Nembo hiyo imetengezwa kuimarisha ujumbe unaotumwa. Nembo hiyo inaonyesha kamera ya kawaida na rangi za upinde wa mvua. Zaidi ya picha milioni 80 na video husambazwa kila siku katika mtandao wa Instagram, mtandao huo una takriban wateja milioni 400 na uliipiku Twitter mwaka 2014.
Viongozi wa mtandao wa Instagram waliiambia Newbeat, “Wakati Instagram ilipokuwa inaanza ilikuwa na eneo la kukarabati na kusambaza picha. Miaka mitano baadaye likawa ni eneo linalopendwa na jamii kubwa ulimwenguni ambapo watu husambaza picha na video.”
Watumiaji pia watagundua kwamba eneo la bluu katika nembo ya mtandao huo limeanza kubadilika na kuwa jeupe. Mtindo huo mpya una lengo la kuimarisha picha na video zinazotumwa bila kubadilisha unavyoingia katika mtandao huo. Ubunifu wa nembo hiyo mpya ulianza mwaka mmoja uliopita.
Aidha walitaka kutengeza nembo ambayo ingewakilisha mahitaji ya awali ya sasa na ya siku za baadaye.


Source: BBC

Saturday, May 7, 2016

VIDEO: Top 10 ya sherehe za gharama zaidi zilizowahi kufanyika, moja ni harusi ya Staa wa Man United

Nimekutana nazo hizi sherehe 10 ambazo zimewahi kuwa na bajeti kubwa zaidi moja katika hizo ipo harusi ya staa wa Machester United Wyne Rooney ambayo imeshika nafasi ya 7 ikiwa na bajeti ya Dola MILIONI 7. #10 Liza Minnelli’s Wedding ~ Bajeti ya dola MILIONI 3.5 #9 Bill Clinton’s Daughter’s Wedding ~ Bajeti ya dola MILIONI 5 […] The post VIDEO: Top 10 ya sherehe za gharama zaidi zilizowahi kufanyika, moja ni harusi ya Staa wa Man United appeared first on TZA_MillardAyo..
 Soma Zaidi>>