Saturday, September 10, 2016

Dully Sykes aongea hiki baada ya Nuh Mziwanda kudai kuibiwa idea ya wimbo ‘Inde’

Baada ya mkali wa wimbo ‘Jike Shupa’ Nuh Mziwanda kudai kuibiwa idea ya wimbo ‘Inde’, Dully Sykes amefunguka na kuzungumzia sakata hilo.



Hivi karibuni Nuh alidai katika maktaba yake ana wimbo ambao unaitwa ‘Inde’ lakini atashindwa kuutoa baada ya kusikia ‘Inde’ ya Dully mtaani huku akimtuhumu producer wake kula njama na Dully Sykes na kutoa idea ya wimbo huo.
Akiongea katika kipindi cha XXL cha Clouds FM Ijumaa hii, Dully Sykes amesema idea ya wimbo ‘Inde’ haikuwa yake, alipewa na Harmonize na yeye kuiboresha zaidi.
“Idea ya ‘Inde’ siyo yangu,” alisema Dully Sykes. “idea ya ‘Inde’ niya Harmonize, nimemkuta nayo mimi nilikuwa sina hata idea hiyo yakusema niimbe ‘Inde’, wala sijui kuhusu maswala ya Inde,”
Alivyoulizwa Harmonize kuhusu idea ya wimbo ‘Inde’ alisema, “Labda mimi nizungumze kitu kimoja, unajua mimi ni msanii mchanga sana, kwanza sina hata miaka 3, siyo kwamba najua sana vitu vingi, lakini vichache navyovijua huwa napenda sana kuweka wazi ili na watu wavijue. Unajua mtu kama Dully Sykes mimi nimeanza kumsikia toka nipo kijijini huko, kila siku anatoa nyimbo, ana hit kibao. Sometime vijana tukiwa tunatafuta angle tutafute angle nzuri kwa sababu kuja kumwambia brother Dully kachua wimbo wako au kaiba, unamvunjia heshima, unaukosea heshima muziki wa bongofleva pia, kwa sababu unavyomzungumzia brother Dully unauzungumzia muziki wa bongofleva, so kumwambia brother Dully wimbo uliotoa na mimi na wimbo wangu wa miaka miwili sijautoa ni kumkosea heshima,” alisema Harmonize.
Wimbo ‘Inde’ wa Dully Sykes unafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya radio na rudinga huku YouTube ukiwa na views milioni moja kwa kipindi cha mwezi mmoja toka utoke.

Wema Sepetu amvutia wire Soudy Brown ‘Man Fongo sio mtu wa kubishana na mama yangu’

Baada ya kusambaa audio katika mitandao ya kijamii ambazo mama Wema anasikika akimpandishia mtangazaji wa Clouds FM, Soudy Brown, Wema Sepetu amemvutia wire mtangazaji huyo akimtaka kuacha kumzungumzia mama yake katika mambo ambayo hayaeleweki.



Chanzo mgogoro huo mkubwa kati ya Wema Sepetu dhidi ya Christian Bella na Man Fongo kwa pamoja, unahusiana na masuala ya show ambazo ‘design’ wamezungukana na mama ameingilia kati!.
Hivyo Soudy kama kawaida yake aliongea na Man Fongo kujua upande wake wa mkasa huo, lakini alijikuta katika wakati mgumu alivyoamua kumpigia mama Wema ili apate chochote kitu kuhusu ubuyu huyo.
Ijumaa hii Wema Sepetu kupitia kipindi cha U Head, aliamua kumtolea uvivu mtangazaji huyo akimtaka kutomwingiza mama yake katika mambo alioyaita yakijinga.
“Soudy hebu acha kumweka mama kwenye hayo mambo, nakuomba mama yangu sijamuweka kwenye hayo mambo, mama yangu ni mtu mzima namweshimu, nakuomba achana na mambo hayo sijui kumpigia simu, sijui maswala ya Man Fongo, nani anamjua Man Fongo?,” aliuliza Wema. “Man Fongo kweli yule wakukaa kubishana na mama yangu, kwa nini mnamrekodi mama yangu hivyo, mimi sipendi,”

Friday, September 9, 2016

Mechi itakuwa ngumu zaidi bila Aguero – Mourinho

Kocha wa klabu ya Man United Jose Mourinho amesema kuwa mechi ya leo dhidi ya mahasimu wao Man City itakuwa ngumu licha ya Sergio Aguero kukosekana.

Thursday, September 8, 2016

NEW VIDEO: G-Lax - SIO KOLOLO

Msanii Mkali chipukizi ameachia video yake mpya wimbo unaitwa #SIOKOLOLO unaweza kuiangalia hapa


    BOFYA LINK HII HAPA CHINI !
     https://www.youtube.com/watch?v=eHAoVr3mQMo

Saturday, September 3, 2016

Ycee amesema haya kwa wasanii bongo na Africa kiujumla

Rapper na muimbaji Nigeria, Ycee amedai kuwa si rahisi kwa wasanii wa Tanzania na hata wa nchi zingine kutoboa Afrika nzima bila kufanya collabo na wasanii wa nchi zingine.

Ycee akiwa na watangazaji wa kipindi cha The Cruise cha East Africa Radio

Baada ya kumuuliza ni wasanii gani wa Tanzania wanafahamika Nigeria na kuwataja Diamod, Alikiba, Vanessa Mdee na Navy Kenzo, nilimuomba atoe ushauri kwa wasanii wengine wanaofanya vizuri lakini hawafahamiki nje ya Afrika Mashariki, Ycee alisema collabo ndio jibu.
Alijitolea mfano mwenyewe kuwa baada ya kuwa kimya na baadaye kurejea kwenye muziki, ili kufahamika kwa wengi ilimlazimu kumshirikisha mtu anayejulikana tayari.
“Nadhani ni kile kile, kama unataka kupenya kwenye soko la Marekani kwa mfano, bila shaka itabidi ufanye kazi na msanii wa Marekani. Kama wamarekani wanatafuta muziki na kuona jina la mtu wasiyemjua ni rahisi kulipita,” alisema.