Baada ya mkali wa wimbo ‘Jike Shupa’ Nuh Mziwanda kudai kuibiwa idea ya
wimbo ‘Inde’, Dully Sykes amefunguka na kuzungumzia sakata hilo.
Hivi karibuni Nuh alidai katika maktaba yake ana wimbo ambao unaitwa
‘Inde’ lakini atashindwa kuutoa baada ya kusikia ‘Inde’ ya Dully mtaani
huku akimtuhumu producer wake kula njama na Dully Sykes na kutoa idea ya
wimbo huo.
Akiongea katika kipindi cha XXL cha Clouds FM Ijumaa hii, Dully Sykes
amesema idea ya wimbo ‘Inde’ haikuwa yake, alipewa na Harmonize na yeye
kuiboresha zaidi.
“Idea ya ‘Inde’ siyo yangu,” alisema Dully Sykes. “idea ya ‘Inde’
niya Harmonize, nimemkuta nayo mimi nilikuwa sina hata idea hiyo
yakusema niimbe ‘Inde’, wala sijui kuhusu maswala ya Inde,”
Alivyoulizwa Harmonize kuhusu idea ya wimbo ‘Inde’ alisema, “Labda
mimi nizungumze kitu kimoja, unajua mimi ni msanii mchanga sana, kwanza
sina hata miaka 3, siyo kwamba najua sana vitu vingi, lakini vichache
navyovijua huwa napenda sana kuweka wazi ili na watu wavijue. Unajua
mtu kama Dully Sykes mimi nimeanza kumsikia toka nipo kijijini huko,
kila siku anatoa nyimbo, ana hit kibao. Sometime vijana tukiwa
tunatafuta angle tutafute angle nzuri kwa sababu kuja kumwambia brother
Dully kachua wimbo wako au kaiba, unamvunjia heshima, unaukosea heshima
muziki wa bongofleva pia, kwa sababu unavyomzungumzia brother Dully
unauzungumzia muziki wa bongofleva, so kumwambia brother Dully wimbo
uliotoa na mimi na wimbo wangu wa miaka miwili sijautoa ni kumkosea
heshima,” alisema Harmonize.
Wimbo ‘Inde’ wa Dully Sykes unafanya vizuri katika vituo mbalimbali
vya radio na rudinga huku YouTube ukiwa na views milioni moja kwa
kipindi cha mwezi mmoja toka utoke.



0 comments:
Post a Comment