Baada ya kusambaa audio katika mitandao ya kijamii ambazo mama Wema anasikika
akimpandishia mtangazaji wa Clouds FM, Soudy Brown, Wema Sepetu
amemvutia wire mtangazaji huyo akimtaka kuacha kumzungumzia mama yake
katika mambo ambayo hayaeleweki.
Chanzo mgogoro huo mkubwa kati ya Wema Sepetu dhidi ya Christian
Bella na Man Fongo kwa pamoja, unahusiana na masuala ya show ambazo
‘design’ wamezungukana na mama ameingilia kati!.
Hivyo Soudy kama kawaida yake aliongea na Man Fongo kujua upande wake
wa mkasa huo, lakini alijikuta katika wakati mgumu alivyoamua kumpigia
mama Wema ili apate chochote kitu kuhusu ubuyu huyo.
Ijumaa hii Wema Sepetu kupitia kipindi cha U Head, aliamua kumtolea
uvivu mtangazaji huyo akimtaka kutomwingiza mama yake katika mambo
alioyaita yakijinga.
“Soudy hebu acha kumweka mama kwenye hayo mambo, nakuomba mama yangu
sijamuweka kwenye hayo mambo, mama yangu ni mtu mzima namweshimu,
nakuomba achana na mambo hayo sijui kumpigia simu, sijui maswala ya Man
Fongo, nani anamjua Man Fongo?,” aliuliza Wema. “Man Fongo kweli yule
wakukaa kubishana na mama yangu, kwa nini mnamrekodi mama yangu hivyo,
mimi sipendi,”



0 comments:
Post a Comment