![]() |
| Ycee akiwa na watangazaji wa kipindi cha The Cruise cha East Africa Radio |
Baada ya kumuuliza ni wasanii gani wa Tanzania wanafahamika Nigeria na kuwataja Diamod, Alikiba, Vanessa Mdee na Navy Kenzo, nilimuomba atoe ushauri kwa wasanii wengine wanaofanya vizuri lakini hawafahamiki nje ya Afrika Mashariki, Ycee alisema collabo ndio jibu.
Alijitolea mfano mwenyewe kuwa baada ya kuwa kimya na baadaye kurejea kwenye muziki, ili kufahamika kwa wengi ilimlazimu kumshirikisha mtu anayejulikana tayari.
“Nadhani ni kile kile, kama unataka kupenya kwenye soko la Marekani kwa mfano, bila shaka itabidi ufanye kazi na msanii wa Marekani. Kama wamarekani wanatafuta muziki na kuona jina la mtu wasiyemjua ni rahisi kulipita,” alisema.
“Ni vile vile pia wasanii kutoka Afrika, si tu Tanzania, hata wasanii wa Nigeria ambao hawajulikani hapa pia wanatakiwa kufanya jitihada hizo pia, kufanya collabo zaidi si tu na wasanii wa nchi yao, bali na wasanii wan chi zingine,” aliongeza.
“Ukimshirikisha mtu kutoka Nigeria, mashabiki wake watasikiliza muziki sababu wanampenda msanii aliyemo kwenye wimbo na vile vile kwa watanzania ambao hawamjui msanii huyo wa Nigeria wataweza kumjua pia msanii huyo.”
Wiki hii Ycee alikuwa na ziara ya siku 3 kuzunguka kwenye vyombo mbalimbali vya habari hapana nchini. Kupitia ziara hiyo amefanikiwa kufanya nyimbo za Weusi pamoja na kundi la Izzo Bizness, The Amazing kishey.blogspot.com/Ycee amesema haya kwa wasanii bongo na Africa kiujumla



0 comments:
Post a Comment