Friday, September 9, 2016

Mechi itakuwa ngumu zaidi bila Aguero – Mourinho

Kocha wa klabu ya Man United Jose Mourinho amesema kuwa mechi ya leo dhidi ya mahasimu wao Man City itakuwa ngumu licha ya Sergio Aguero kukosekana.


Aguero atakosa mechi hiyo kufuatia kufungiwa kucheza mechi 3 baada ya kumpiga kiwiko beki Weiston Reid wa West Ham.
Mchezaji huyo kutoka Argentina amefunga goli 6 katika mechi 4 za City msimu huu lakini Jose anaamini kukosekana kwake kutafanya kuwa vigumu kutabiri mbinu za Pep Guardiola.
“Aguero akiwepo inakuwa ni vigumu ,Bila ya Aguero inakuwa ni vigumu zaidi” amesema Kocha huyo wa Man United alipo kuwa akizungumza na waandishi wa habari.
“Lakini wana kikosi kipana ,anaweza kumchezesha Kelechi Iheanacho,Sterling au Silva kama namba 9 wa uongo ” amesema Jose
Aidha kwa upande mwingine kocha huyo amesema hana majeruhi ” hakuna majeruhi, hakuna ambaye yupo nje ya mchezo. Kwa hiyo tupo salama,tupo tayari. Tunasubiri”

0 comments:

Post a Comment