Friday, May 13, 2016

Hatuangalii ukubwa wa jina la msanii - Mafikizolo

kundi la muziki kutoka South Afrika Mafikizolo wamesema kolabo inaweza kumyanyua mtu katika muziki na kufanya akawa na nafasi nzuri kimataifa kwa hiyo kolabo ni kitu kizuri kwa wasanii.

                                          kundi la muziki kutoka South Afrika Mafikizolo
 
     
Wakizungumza na Enewz Mafikizolo wamesema kuwa kwa wasanii wanaohitaji kolabo na kundi lao wao hawaangalii ukubwa wa jina la msanii bali wanachokiangalia radha ya msanii na uwezo wa mtu katika kuimba.
“Huwa hatuangalii jina la msanii sisi tukipenda tu radha ya msanii tunafanya nae kolabo na hivyo ndivyo wasanii wengine wanapaswa kuviangalia”,walisema Mafikizolo.
Huku wakitolea mfano walivyowapa nafasi uhuru na Maphorisa na kuwaweka juu katika ramani ya muziki wakati walikuwa hawatambuliki katika game ya muziki lakini wao waliweza kuwafanya wao kutambulika na wengine kuanza kuomba kolabo kwao.

Ungana nami Kishey Platnumz sasa
Jiunge nami kupitia Facebook, twitter na Instagram upate update za kijanja!

0 comments:

Post a Comment