Msanii wa muziki kutoka label ya ‘High Table Sound’ ya Barnaba, ‘Ice
Boy’ amefunguka na kuzungumzia maisha yake ya muziki pamoja na mipango
yake akiwa ndani ya label hiyo.
Akizungumza na Bongo5, Ice Boy amesema anaamini ‘High Table Sound’ inaweza kubadili maisha yake ya muziki.“Kwa sasa nipo kwa Barnaba, tayari nimeona wapi natakiwa kwenda na
kwa njia gani,” alisema Ice Boy. Kwa hiyo naweza sema hapa kwangu ni
sehemu sahihi kwangu, tayari kuna kolabo za kimataifa nimefanya, kwa
hiyo mashabiki wakae mkao wa kula kuna mambo mengi mazuri yanakuja,”
alisema Ice Boy.



0 comments:
Post a Comment