Saturday, September 10, 2016

Dully Sykes aongea hiki baada ya Nuh Mziwanda kudai kuibiwa idea ya wimbo ‘Inde’

Baada ya mkali wa wimbo ‘Jike Shupa’ Nuh Mziwanda kudai kuibiwa idea ya wimbo ‘Inde’, Dully Sykes amefunguka na kuzungumzia sakata hilo.



Hivi karibuni Nuh alidai katika maktaba yake ana wimbo ambao unaitwa ‘Inde’ lakini atashindwa kuutoa baada ya kusikia ‘Inde’ ya Dully mtaani huku akimtuhumu producer wake kula njama na Dully Sykes na kutoa idea ya wimbo huo.
Akiongea katika kipindi cha XXL cha Clouds FM Ijumaa hii, Dully Sykes amesema idea ya wimbo ‘Inde’ haikuwa yake, alipewa na Harmonize na yeye kuiboresha zaidi.
“Idea ya ‘Inde’ siyo yangu,” alisema Dully Sykes. “idea ya ‘Inde’ niya Harmonize, nimemkuta nayo mimi nilikuwa sina hata idea hiyo yakusema niimbe ‘Inde’, wala sijui kuhusu maswala ya Inde,”
Alivyoulizwa Harmonize kuhusu idea ya wimbo ‘Inde’ alisema, “Labda mimi nizungumze kitu kimoja, unajua mimi ni msanii mchanga sana, kwanza sina hata miaka 3, siyo kwamba najua sana vitu vingi, lakini vichache navyovijua huwa napenda sana kuweka wazi ili na watu wavijue. Unajua mtu kama Dully Sykes mimi nimeanza kumsikia toka nipo kijijini huko, kila siku anatoa nyimbo, ana hit kibao. Sometime vijana tukiwa tunatafuta angle tutafute angle nzuri kwa sababu kuja kumwambia brother Dully kachua wimbo wako au kaiba, unamvunjia heshima, unaukosea heshima muziki wa bongofleva pia, kwa sababu unavyomzungumzia brother Dully unauzungumzia muziki wa bongofleva, so kumwambia brother Dully wimbo uliotoa na mimi na wimbo wangu wa miaka miwili sijautoa ni kumkosea heshima,” alisema Harmonize.
Wimbo ‘Inde’ wa Dully Sykes unafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya radio na rudinga huku YouTube ukiwa na views milioni moja kwa kipindi cha mwezi mmoja toka utoke.

Wema Sepetu amvutia wire Soudy Brown ‘Man Fongo sio mtu wa kubishana na mama yangu’

Baada ya kusambaa audio katika mitandao ya kijamii ambazo mama Wema anasikika akimpandishia mtangazaji wa Clouds FM, Soudy Brown, Wema Sepetu amemvutia wire mtangazaji huyo akimtaka kuacha kumzungumzia mama yake katika mambo ambayo hayaeleweki.



Chanzo mgogoro huo mkubwa kati ya Wema Sepetu dhidi ya Christian Bella na Man Fongo kwa pamoja, unahusiana na masuala ya show ambazo ‘design’ wamezungukana na mama ameingilia kati!.
Hivyo Soudy kama kawaida yake aliongea na Man Fongo kujua upande wake wa mkasa huo, lakini alijikuta katika wakati mgumu alivyoamua kumpigia mama Wema ili apate chochote kitu kuhusu ubuyu huyo.
Ijumaa hii Wema Sepetu kupitia kipindi cha U Head, aliamua kumtolea uvivu mtangazaji huyo akimtaka kutomwingiza mama yake katika mambo alioyaita yakijinga.
“Soudy hebu acha kumweka mama kwenye hayo mambo, nakuomba mama yangu sijamuweka kwenye hayo mambo, mama yangu ni mtu mzima namweshimu, nakuomba achana na mambo hayo sijui kumpigia simu, sijui maswala ya Man Fongo, nani anamjua Man Fongo?,” aliuliza Wema. “Man Fongo kweli yule wakukaa kubishana na mama yangu, kwa nini mnamrekodi mama yangu hivyo, mimi sipendi,”

Friday, September 9, 2016

Mechi itakuwa ngumu zaidi bila Aguero – Mourinho

Kocha wa klabu ya Man United Jose Mourinho amesema kuwa mechi ya leo dhidi ya mahasimu wao Man City itakuwa ngumu licha ya Sergio Aguero kukosekana.

Thursday, September 8, 2016

NEW VIDEO: G-Lax - SIO KOLOLO

Msanii Mkali chipukizi ameachia video yake mpya wimbo unaitwa #SIOKOLOLO unaweza kuiangalia hapa


    BOFYA LINK HII HAPA CHINI !
     https://www.youtube.com/watch?v=eHAoVr3mQMo

Saturday, September 3, 2016

Ycee amesema haya kwa wasanii bongo na Africa kiujumla

Rapper na muimbaji Nigeria, Ycee amedai kuwa si rahisi kwa wasanii wa Tanzania na hata wa nchi zingine kutoboa Afrika nzima bila kufanya collabo na wasanii wa nchi zingine.

Ycee akiwa na watangazaji wa kipindi cha The Cruise cha East Africa Radio

Baada ya kumuuliza ni wasanii gani wa Tanzania wanafahamika Nigeria na kuwataja Diamod, Alikiba, Vanessa Mdee na Navy Kenzo, nilimuomba atoe ushauri kwa wasanii wengine wanaofanya vizuri lakini hawafahamiki nje ya Afrika Mashariki, Ycee alisema collabo ndio jibu.
Alijitolea mfano mwenyewe kuwa baada ya kuwa kimya na baadaye kurejea kwenye muziki, ili kufahamika kwa wengi ilimlazimu kumshirikisha mtu anayejulikana tayari.
“Nadhani ni kile kile, kama unataka kupenya kwenye soko la Marekani kwa mfano, bila shaka itabidi ufanye kazi na msanii wa Marekani. Kama wamarekani wanatafuta muziki na kuona jina la mtu wasiyemjua ni rahisi kulipita,” alisema.

Wednesday, June 8, 2016

Queen Darleen asema alikuwa mfanyakazi ndani ya ‘WCB’ kabla ya kusaini kama msanii

Msanii wa muziki ambaye pia ni dada wa staa wa muziki Diamond Platnumz, Queen Darleen baada ya kusaini WCB hivi karibuni, amefunguka na kueleza jinsi alivyokuwa ananufaika na mafanikio ya kaka yake.































Akizungumza na Bongo5 Jumatatu hii, Queen Darleen amesema alikuwa ni mfanyakazi wa kawaida ndani ya WCB na alikuwa akilipwa mshahara kama wafanyakazi wengine.
“Kabla ya kusaini WCB maisha yangu yalikuwa yameshabadilika,” alisema Darleen “CEO tayari alikuwa ameshanibadilishia maisha yangu, nilikuwa nafanya kazi mbalimbali ndani ya WCB na nilikuwa nalipwa, kama zile behind the scenes nilikuwa nazisimamia mimi,”
Muimbaji huyo amezungumzia hatua ya kusaini ‘WCB’.
“WCB ni label ambayo inafanya poa kwa sasa, kwa hiyo kufanya kazi chini ya ‘WCB’ ina maana kwamba muziki wangu sasa unaenda katika level nyingine, hii ni hatua nzuri, tuombe Mungu mambo yaende vizuri, muziki wangu utafika mbali zaidi, kwa hiyo mashabiki wakae mkao wa kula kwa ajili ya vitu vipya na vizuri, nini ndiye Queen ‘WCB’,” alisema Darleen.

KISHEY PLATNUMZ!

Rich Mavoko adai kuwa kuna msanii mkubwa wa Bongo alimuambia asisaini WCB

RICH MAVOKO
Sio watu wote waliofurahia Rich Mavoko kusainiwa chini ya label ya WCB, ikiwemo wasanii wengine wakubwa wa Bongo Fleva.
Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo, Mavoko amedai kuwa kuna msanii alimkataza kusainiwa chini ya label hiyo inayomilikiwa na Diamond Platnumz baada ya taarifa za yeye kusainiwa kwenye label hiyo kutoka.
WCB WASAFI           

“Sijawahi kusema hili ila ukweli ni kwamba wakati nataka kwenda WCB kuna msanii mkubwa alinitumia ujumbe na kuniambia Rich Mavoko unakwendaje kusimamiwa kazi zako na Diamond Platnumz ” Mavoko alifunguka. “Kiukweli aliniumiza sana ila nilimjibu kwa roho moja kuwa brother wewe hujui mimi nimetoka wapi na nakwenda wapi hivyo huwezi kujua hata hili litakujae kwangu.”

Rich Mavoko tayari ameachia wimbo wa kwanza akiwa chini ya label hiyo, Ibaki Story ambayo inazidi kufanya vizuri kwenye media mbali mbali vikiwemo TV na RADIOS.

KISHEY PLATNUMZ!