Wednesday, June 8, 2016

Queen Darleen asema alikuwa mfanyakazi ndani ya ‘WCB’ kabla ya kusaini kama msanii

Msanii wa muziki ambaye pia ni dada wa staa wa muziki Diamond Platnumz, Queen Darleen baada ya kusaini WCB hivi karibuni, amefunguka na kueleza jinsi alivyokuwa ananufaika na mafanikio ya kaka yake.































Akizungumza na Bongo5 Jumatatu hii, Queen Darleen amesema alikuwa ni mfanyakazi wa kawaida ndani ya WCB na alikuwa akilipwa mshahara kama wafanyakazi wengine.
“Kabla ya kusaini WCB maisha yangu yalikuwa yameshabadilika,” alisema Darleen “CEO tayari alikuwa ameshanibadilishia maisha yangu, nilikuwa nafanya kazi mbalimbali ndani ya WCB na nilikuwa nalipwa, kama zile behind the scenes nilikuwa nazisimamia mimi,”
Muimbaji huyo amezungumzia hatua ya kusaini ‘WCB’.
“WCB ni label ambayo inafanya poa kwa sasa, kwa hiyo kufanya kazi chini ya ‘WCB’ ina maana kwamba muziki wangu sasa unaenda katika level nyingine, hii ni hatua nzuri, tuombe Mungu mambo yaende vizuri, muziki wangu utafika mbali zaidi, kwa hiyo mashabiki wakae mkao wa kula kwa ajili ya vitu vipya na vizuri, nini ndiye Queen ‘WCB’,” alisema Darleen.

KISHEY PLATNUMZ!

Rich Mavoko adai kuwa kuna msanii mkubwa wa Bongo alimuambia asisaini WCB

RICH MAVOKO
Sio watu wote waliofurahia Rich Mavoko kusainiwa chini ya label ya WCB, ikiwemo wasanii wengine wakubwa wa Bongo Fleva.
Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo, Mavoko amedai kuwa kuna msanii alimkataza kusainiwa chini ya label hiyo inayomilikiwa na Diamond Platnumz baada ya taarifa za yeye kusainiwa kwenye label hiyo kutoka.
WCB WASAFI           

“Sijawahi kusema hili ila ukweli ni kwamba wakati nataka kwenda WCB kuna msanii mkubwa alinitumia ujumbe na kuniambia Rich Mavoko unakwendaje kusimamiwa kazi zako na Diamond Platnumz ” Mavoko alifunguka. “Kiukweli aliniumiza sana ila nilimjibu kwa roho moja kuwa brother wewe hujui mimi nimetoka wapi na nakwenda wapi hivyo huwezi kujua hata hili litakujae kwangu.”

Rich Mavoko tayari ameachia wimbo wa kwanza akiwa chini ya label hiyo, Ibaki Story ambayo inazidi kufanya vizuri kwenye media mbali mbali vikiwemo TV na RADIOS.

KISHEY PLATNUMZ!

KENYA YAKOSA UMEME TAKRIBANI SIKU NNE KISA NI.....


Kampuni ya kuzalisha umeme nchini Kenya, KENGEN imetuma taarifa kwa vyombo vya habari ikiomba radhi kwa ukosefu wa umeme Kwa hapo jana.
Hilo sio jambo geni.
Mara kwa mara umeme hupotea nchini Kenya kwa sababu moja au nyengine, sawa tu na mataifa yote barani Afrika
Hata hivyo sababu walioitoa KENGEN kwa ukosefu huo wa umeme Kwa takriban saa nne kote nchini humo ndio imewaacha wengi wamepigwa na butwaa !

Nyani.


Amini usiamini, KENGEN imempata nyani mmoja katika eneo maalum lenye 'swichi' hiyo katika mtambo wa kuzalisha umeme ulioko kwenye bwawa kuu la Gitaru Mashariki mwa Kenya.
Sasa kampuni hiyo inasema huenda nyani huyo ndiye aliyezima umeme kote nchini Kenya !
Kengen inasema kuwa huenda nyani huyo aliangukia mashine hiyo ndogo na ''kusababisha hitilafu ya takriban megawati 180 za umeme ambao ndio uliosababisha ukosefu wa umeme kote nchini Kenya.''

 Kwa takriban saa nne taarifa hiyo ilielezea.

Tumbili huyo alinusurika na sasa amechukuliwa na shirika la huduma kwa wanyama pori KWS ilikupokea matibabu.
"mitambo ya kuzalisha umeme kote nchini Kenya huwa imezingirwa na nyaya za umeme ilikuwazuia wanyama wa porini kuingia humo na kusababisha madhara kama hayo ya jana , taarifa hiyo ilisema.
''Tunaomba radhi kwa tukio hilo la kipekee la hapo jana na sasa tumeanza kuweka mikakati dhabiti ya kuzuia marudioa ya ajali hiyo'' taarifa hiyo ya KenGen ilielezea.
Mashirika mengi pamoja na wawekezaji wa kibinafsi walilazimika kufunga biashara zao hapo jana huku wale waliokuwa na nitambo binafsi za kuzalisha umeme wakiingia gharama zaidi ya kununua mafuta .
Wakenya wengi waliopokea habari hizo waliikejeli kampuni hiyo ya kuzalisha umeme wengi wakiwatania katika mitandao ya kijamii.

KISHEY PLATNUMZ!

Tuesday, June 7, 2016

Entertainment Picha,Jumba lililotumika kuhifadhi mwili wa bondia Muhammad Ali linavyolindwa.

HAYATI MOHAMAD ALI
Jumba lililotumika kuhifadhi mwili wa bondia Muhammad Ali limeonekana kulindwa vikali na timu ya askari tofauti.

Mashaidi mjini Louisville, Kentucky wameona zaidi ya magari matatu ya polisi nje ya jumba hilo la A.D. Porter & Sons. Askari hao ni kutoka kikosi cha Jefferson County Sheriff na Louisville Metro PD.

Msemaji wa nyumba hio ya kuhifadhi maiti amesema polisi wapo hapo kuzuia fujo kutoka kwa mashabiki na wapenzi pamoja na kulinda mwili wa bondia huyo.

Muhammad Ali anazikwa ijumaa hii.

Friday, June 3, 2016

Ronaldinho kutokea kwenye filamu mpya ya Van Damme

Staa wa soka duniani, Ronaldinho Gaucho amekubali kucheza kwenye filamu mpya ya kikckboxer ‘Retaliation’ ya Jean-Claude Van Damme.

RONALDINHO AKIWA ON SET
   
Ronaldinho ambaye kwenye filamu hiyo ametumia jina la Ronaldo atakuwa pamoja na mastaa wengine kama Mike Tyson, Fabricio Werdum na Paige Van Zant.
Producer Rob Hickman kutoka Hollywood amesema, “As producers, much like advertisers and brands, we must look at a potential star’s total value. In addition to his charisma, Ronaldinho also brings with him 66 million social media followers from all parts of the globe. Those numbers are an element that a lot of traditional movie stars can’t offer and when we market the film, that is something that will be invaluable.”

 Jiunge na kishey Platnumz sasa!

Friday, May 27, 2016

M 2The P aeleza kilichotokea siku Ngwea anafariki, adai anahisi kuna mkono wa mtu

Msanii wa muziki M 2The P ambaye alikuwa rafiki mkubwa wa msanii Albert Mangwea, amesema hadi leo anahisi kuna mtu aliyehusika na kifo cha Ngwea, na kumfanya ashindwe kuamini ni ajali ya kawaida.

MSANII M 2THE P AKIWA NA HAYATI NGWAIR

Akiongea katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio Ijumaa hii, M2The P amesema kitendo cha kuibiwa vitu vyao vyote ndio kilichompa wasi wasi.
“Unajua ile siku tuli-party sana,” alisema M2 The P. “ Tumepiga bata lakini kilichonishtua, ni sawa tukio lilikuwa kama ilivyoonekana ila kilichonishangaza ni baada ya kurudi ghetto tukakuta vitu vyote vimeibiwa, kitu kilichonishtua, ina maana ilikuwa ni kama walitu-target kabisa,”
Pia msanii huyo ambaye naye siku ya tuko hakuwa katika hali nzuri baada ya kupoteza fahamu, amesema kulingana na hali hiyo, anaunga mkono kauli ya mama mzazi wa Ngwea Bi. Denisia Constantino, kwamba huenda kuna watu walishiriki kusababisha kifo cha Ngwea.

Friday, May 20, 2016

Diamond kwenye headlines nyingine na Wizkid, AKA, Drake, Beyonce na Rihanna

   
   
May 20 2016 Tanzania imeamka na habari nyingine njema za Diamond Platnumz kuchaguliwa tena kushiriki kwenye tuzo za kituo maarufu cha TV Marekani kiitwacho BET ambapo Platnumz amekua na mwaka mwingine mfululizo wa kuwa nominated na sasa ni kwenye tuzo za BET Awards 2016.
Diamond ameshukuru kwa kuchaguliwa kuwania tuzo kwenye kipengele cha Best international Act Africa ambapo ameyaandika maneno haya baada ya kufikiwa na taarifa >>> ‘Ningependa niwashukuru kwa Sapoti kubwa Manayozidi kunipa na niwajuze kuwa kijana wenu nimechaguli kuwania tunzo ya Msanii Bora wa Kimataifa toka Africa kwenye tunzo za BET #BETAwards America’
Tuzo za BET 2016 ambazo zitatolewa nchini Marekani zimeanza kuchukua nafasi kwenye headlines baada ya kutangazwa list ya waliochaguliwa kuwania huku Beyonce, Rihanna na Drake wakitangazwa kuongoza kwa kuwania tuzo zaidi ya moja.






  BET 2